Walimu Waikomalia Serikali Madai Yao..!!!


Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Mara, Livingstone Gamba amesema licha ya walimu kupiga kelele kila mara, Serikali imekaa kimya kuhusiana na malimbikizo ya madai wanayoidai.

Gamba amesema wataendelea kupiga kelele bila kuchoka kwa kuwa wanachodai ni haki yao ya msingi na kwamba, jasho lililowatoka ndilo wanalolipigania.

Wakati kigogo huyo akisema hayo, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Tarime kimetangaza ‘mshiko’ wanaoidai Serikali umefikia Sh399 milioni.

Akizungumza kwenye mkutano wa kamati tendaji ya chama hicho wilayani Tarime, Mwenyekiti wa CWT wa wilaya hiyo, Shirikisho Nyagoseima amesema madai hayo ni matibabu (Sh30 milioni), likizo (Sh20. 6 milioni), masomo (Sh22.7 milioni), uhamisho (Sh183.8 milioni), mazishi (Sh6.3 milioni), usafirishaji mizigo (Sh20 milioni) na mishahara yanayofikia Sh245.3 milioni.

 “Tunaitaka Serikali kulipa stahiki hizi ili walimu wafanye kazi kwa kiwango kinachotakiwa ifikapo Machi Mosi ili tusiingie kwenye mgogoro,” amesema Nyagoseima.

Tayari Rais wa CWT ngazi ya Taifa, Gratian Mkoba ametangaza kuwa chama hicho kinatarajia kutangaza mgogoro na Serikali ifikapo mwezi ujao iwapo malimbikizo ya madai ya walimu yatakuwa hayajalipwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad