Wamempingaaah..Wenye Maduka ya Kubadili Fedha Dar Watoa Kauli Hii Nzito Juu ya Makonda..!!


 Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza kuwa kuna maduka mengi ya kubadili fedha (Bureau de Change) ambayo yanatumika kutakatisha fedha za dawa za kulevya, wasimamizi wa maduka hayo wameeleza kutoshiriki, bali wanafuata utaratibu uliowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa nyakati tofauti wamesema kabla ya kuuza au kununua fedha za ndani na nje ya nchi, hupewa utaratibu ambao ni lazima waufuate.

Akizungumza juzi wakati wa kukabidhi majina 97 ya watuhumiwa wa uuzaji wa dawa za kulevya, Makonda amesema jijini Dar es Salaam kuna maduka ya kubadilishia fedha takriban 220 na nchi nzima yapo zaidi ya 400, hivyo utitiri wa maduka hayo unarahisisha kuingiza fedha za dawa za kulevya kwenye mzunguko na kusaidia kutakatisha fedha haramu.

Meneja wa duka la kubadilishia fedha la TK, Tukuza Amri amesema ndiyo kwanza amesikia tuhuma hizo kwa sababu wao hufuata kanuni na utaratibu wa BoT.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Anataka sote tukatengeneze garden majumbani kwake

    ReplyDelete
  2. Huyu meneja asemekama yeye , je anawajuwa wenzake wenye maduka hayo. Namhakikishia kuwa Mhe, Makonda yupo sahihi, CARTEL za madawa ya kulevya hawawezi kurahisisha biashara zao bila kuwa na uhakika wa kupata fedha za kigeni, ni kwa sababu kasema Makonda na anaonekana kama anaonea, ukweli ndiyo huo. Wauza madawa ya kulevya walishauza kwa fedha za kitanzania na wanahitaji kwenda nje ya Tanzania kununua madawa hayo wanatumia fedha zipi kama siyo za kigeni?uenda hata wao wanahusika katika network hizo ili kulahisisha upatikanaji wa fedha kwa wanunuzi na wasmbazaji wa dawa za kulevya.

    ReplyDelete
  3. kila mwenye duka ajitetee peke yake, asiwasemee wenzake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad