Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania.
Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.
"Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana". Amesema Wema Sepetu
Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.
"Sijachukua pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike" - Amesema Wema
Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" - Wema Sepetu
Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia amerudisha kadi ya CCM kusema
"Tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo CCM haikumtendea haki
Kuhusu sauti zilizosambazwa mitandani zikionesha Mama Wema akiongea na Steve Nyerere, mama Wema amesema "Kuhusu sauti zinazosemwa kuwa ni mimi na Steve Nyerere, siwezi kulizungumzia hilo maana sijazisikia"
Wewe wasema lakini mama kasema uliahudiwa dola 200,000/ kwa nini leo iwe burebure?haingii akilini.
ReplyDeleteHuko sasa pouwa, utavuta bangi kwa raha zako, hakuna wa kuku-uliza, wanasheria wapo kibao wa-kukutetea.....ppiiiiippoooooozz PWAAAAAAA!!
ReplyDeleteNchi haina sababu yoyote ya kufurahia haya yanayotokea.
ReplyDeleteWa kubwia imekuwa ni saratani inayolitesa taifa. Tuwe macho saratani hii isiingie hatua ya tatu tatu na ya nne. Tutashindwa kuitibu iangamize taifa.
dada umefanya haraka, ungetulia kwanza!
ReplyDeleteMbona wengi wanahama vyama hawajitangazi? Huna impact yoyote na kula yako itafidiwa na mwanangu aliyetimiza miaka 18
ReplyDeletehaya mama safari njema uko uendako
ReplyDeleteila ningekushauri ufocus sana kwenye carrier yako ya sanaa
na uachane na siasa kwani hazikufai
na hata hvyo kuondoka kwako ccm sidhani kama kuna pengo lolote
coz unaonekana uko kwenye siasa kwa maslai binafsi na si kwa ajili ya wananchi
si bora ungeenda ACT wazalendo
ReplyDeleteNjaa mbaya jamani😂😂😂ameshindwa kumtoa Zari madale ataweza kumtoa Magufuli Magogoni?!
ReplyDeleteEti demokrasia ahahaaa kwa maslahi yako mwenyew ndo unasem dekmokrasia. Jarib ila umekurupuk kwa uamuz ulio ufany na utajuta badaae. Kwa kweli unawashauri? Sidhani.
ReplyDeleteSiasa ziliisha toka 20 15 muda huu mtu a hame au asihame siyo ishu. Cha msingi tuombe Mungu nchi iwe na amani na haki itendeke katika kila nyanja ya Serikali.
ReplyDeleteTupate huduma zote zinazostahili kutolewa na Serikali na hali ya maisha iboreshwe.
Wanaohama wahame tu ila taifa lisonge mbele.Hicho ndo kitu cha msingi
Tufahamu tu kuwa hakuna mkamilifu. Na kila binadamu ana haki sawa mbele ya Mungu.
Mungu Ibariki Tanzania.
mbona povuu. kwani nn ni family ya Wema auxxx. pesa apate mwingine nyini mkauke midomo. poleni
ReplyDeleteHivi tangu lini huyo malaya alianza siasa???? Mimi nilifikiria ni muuza sura wa Bongo Movie kumbe ni Mwanasiasa??? Dah!!!.....Karibu sana huku kilingine kwani ndio kwaaanzaaa kumekucha. Karibu sana huku na wewe uyaone. Ulikuwa unayasikia tu lakini kwa sasa ndio utayaona mwenyewe. Ili mradi umedhamiria kuyavulia maji nguo ni sharti uyaoge. Usije kukimbia tu kwani hutakuwa mgeni wa mtu yoyote yule. Na pia wakaribishe tena kwa moyo mkunjufu wale mashabiki wako wooooteee na zile Likes zoooote za kwenye Instagram. Zote zilete huku kijiweni. Hakikisha unafanya juhudi kubwa za kuwaleta ili tukomae pamoja huku. Wasiiishie tu kwenye kuku follow na ku like mambo yako kinafiki. Hakikisha na wao wameunga tela ili tushirikiane kwa pamoja. Ni wosia tu kwako mdada mwanasiasa.
ReplyDeletemmh na huyo nae mama mtu mzima huoni hata haya kuingizwa kwenye mamedia kqmq motto mdogo hebu jiheshimu sijui kama mume wako angekuwepo ingekuwaje si mngemtia aibu mzee wa watu maana loooooooooo
ReplyDelete