Wema Sepetu Afunguka Mazito Baada ya Jana Jina Lake Kuyajwa Kuwa Anahusika na Madawa ya Kulevya..!!!


Staa huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwenye orodha ya mastaa wanaotuhumiwa kubwia unga na walioamriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujisalimisha kituo cha polisi central jijini Dar, Ijumaa hii kwa mahojiano zaidi.

“Mimi kama Wema nimekuwa nikisemwa sana kuhusu kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kujihusisha katika kuuza madawa ya kulevya,” amesema Wema kupitia app yake.

“Sometimes wanasema nimefungwa, sometimes nimenyongwa, sometimes nimekamatwa hususan pindi ninaposafiri kwenda nchi mbalimbali, na sasa hivi nimeambiwa kwamba natumia madawa ya kulevya. Well, ni habari ambazo mheshimiwa mkuu wa mkoa amesema hana uthibitisho nazo lakini amelazimu kutaja majina kadha wa kadha ambayo ndio hivyo ameyataja mengine kwenye vyombo vya habari, na ameamuru twende tukaripoti kesho (leo Feb 3), ifikapo saa tano asubuhi,” ameongeza.

“Mi nasema hivi, nitaenda, nitaripoti, kwasababu ni wito ambao ametaja mkuu wa mkoa wangu kuona amefanya, unaambiwa kubali wito, usikatae neno. Kwahiyo tutaenda kesho, na ntamsikiliza yale ambayo anataka kuniambia, iwapo tukishajua which is true, which is not, then tutajua from there what to do, sasa hivi sina cha kusema, sina cha kufanya, because bado sijaonana naye, kwa sasa niacheni tu nirelat but I want to assure you one thing, I am not a drug addict, and I am not a drug abuser, and if I was nadhani we all know how drug addicts act, we all know how drug abusers wanakuwaga. I want you guys to relax, do not worry, everything is going to be fine.”

Mastaa wengine waliotajwa ni TID, Mr Blue, Chidi Benz, Recho na wengine.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tunakuamini Wema waache wanaokuchukia watukane ila cku yao itafika. usijali umaarufu na roho yako nzuri ndo inakuponza. kumbuka hata mtume Muhammad (AWS) nae alipata matatizo kwa kuutangaza uislam. na bado aliwaombea kwa Allah awasamehe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kumfananisha mtume wetu na huyo mpuuzi mwenzio

      Delete
    2. Roho nzuri ya kugawa kipapa au ? @ Anonymous 8;10

      Delete
  2. do not worry Wema duniani huwezi kuishi bila matatizo, tunajua ni uongo wa hali ya juu. niya yao kukuchefua tuu. swala na dua zetu zitafika kwa ALLAH

    ReplyDelete
  3. Unakubali upimwe kama unatumia unga. Nasema vipimo vya uhakika ( Kupimwa nywele au wataalamu wa nje wasio pokea ongo.) Ukweli ni huo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad