Wema Sepetu amchinjia baharini Batuli


Sasa Wema Sepetu na Batuli ni mbuzi na chui, urafiki ndio umefika mwisho. Tukio hilo limetokea baada ya Wema kukasirishwa na kitendo cha Batuli kusema kuwa yeye alishalipwa fedha zake za kampeni na CCM.

Kupitia mtandao wa Instagram, Wema Sepetu ameweka picha ya rafiki yake huyo wa zamani na kuandika ujumbe ambao umeashiria kuwa urafiki wao ndio basi tena.


“Neno Moja Kwake…! Temporary Post… Mimi naanza… Alikuwa Rafiki yangu na Tulipendana sana….,” ameandika Wema kwenye picha ya Batuli hiyo hapo juu aliyoiweka kwenye mtandao huo.

Baada ya ujumbe huo wa Wema, Nay wa Mitego amemchochea muigizaji huyo ambaye wote kwa sasa wanakisupport Chadema kwa kuandika, “ @wemasepetu #MudaWetu Wana Maneno Mengi Tatizo Hawa Action… Usi mwamini ndugu Ata Rafiki, wachukulie Wote wanafiki, ishi tu kivyako Binadamu awa aminiki..! 

Bongo5

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kichwa cha habari kizito kachinjiwa baharini dah nyie waandishi too much kuliko habari yenyewe imekosa miguu wala kichwa

    ReplyDelete
  2. KWELI KAKURUPUKA,NA ATAJIJU YY NA BIBI YAKE..

    ReplyDelete
  3. sasa akipotea njia si atarekibishwa wacheni majungu wema kuhamia chadema
    maneno mengi hsta rafiki anageuka kuwa adui muacheni kwa raha zake kamua na anaetaka he or she they are all welcome ila maneno maneno uchonganishi acheni just because kasema ukweli basi mumpige vita steve pia cos yeye ndie aliwatumbua wote

    ReplyDelete
  4. MPUUZI WEMA,ANGESUBIRI AU ANGEJICHOMOA MAPEMA.KWA MUDA HUU TUNAAMINI NI HASIRA ZA KUTUHUMIWA NA MADAWA.

    ReplyDelete
  5. Mimi sina chama wala sipigi kura, lakini kwa mtazamo wangu naona haiwezekani mtu uzunguuke nchi nzima ufanye kampeni halafu usilipwe, kweli inaingia akilini hiyo? yaani upoteze muda wako jua lako mvua yako umo majiani tuu halafu usilipwe kitu utakubali kweli? halafu uchaguzi haujaisha leo wala jana leo ndio unasema hujalipwa baada ya sakata la madawa? kama kweli hajalipwa wema hawezi kukaa na jambo angelikuwa keshasema zamani sio sasa mwaka wa pili ndio unasema tena baada ya msala wa madawa.

    ReplyDelete
  6. Mimi sina chama wala sipigi kura, lakini kwa mtazamo wangu naona haiwezekani mtu uzunguuke nchi nzima ufanye kampeni halafu usilipwe, kweli inaingia akilini hiyo? yaani upoteze muda wako jua lako mvua yako umo majiani tuu halafu usilipwe kitu utakubali kweli? halafu uchaguzi haujaisha leo wala jana leo ndio unasema hujalipwa baada ya sakata la madawa? kama kweli hajalipwa wema hawezi kukaa na jambo angelikuwa keshasema zamani sio sasa mwaka wa pili ndio unasema tena baada ya msala wa madawa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad