Zilizotufikia Hivi Punde..Masogange Ndaniii Akamatwa na Polisi Sakata la Madawa ya Kulevya..!!!


TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba video queen maarufu Bongo, anayefahamika kutokana na shepu yake matata, Agness Gerald almaarufu Masogange, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba, mpaka muda huu bado anashikiliwa central. Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu Bongo, walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na ishu ya matumizi na biashara ya madawa ya kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange na kinachoendelea, zitaendelea kukujia kupitia hapahapa, endelea kufuatilia mtandao huu na pia kufuatilia Udaku Special Blog

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. usichezee mkono wa sirikali.... dangerous...

    ReplyDelete
  2. Haya mambo ya 'kimya-kimya' yamepitwa na wakati, sasa hapo hatuna uhakika kama ni kweli ama la, lakini ingetajwa ile list ya watu 97, tungejiridhisha hata kwa hili pia...........anyway, tutafanyaje sasa, YETU MACHO!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad