Zitto Aibua Tafrani Bungeni,Aongoza Wenzake Kutoka Nje ya Bunge...!!!


Wabunge wa upinzani watoka nje ya Bunge kumpinga kukamatwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA)  Tundu Lissu.

Wabunge hao wametoka nje ya Bunge hivi punde baada ya Naibu Spika kumtaka Mbunge wa Serengeti kutoka nje baada ya kutokea mabishano yaliyotokana na hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) ya kutaka Bunge lijadili swala Haki na Madaraka ya Bunge kukiukwa kwa wabunge kukamatwa ndani ya viwanja vya Bunge kinyume na utaratibu.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amewatoa nje ya Bunge, wabunge watatu wa CHADEMA, Halima Mdee (Kawe), Esther Bulaya (Bunda) na Marwa Ryoba (Serengeti).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad