Zitto Kabwe Ashindwa Kuzuia Hisia Zake Sakata Kushikiliwa Godbless Lema...Ataka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Iwajibishwe


Kitendo cha Mbunge wa Arusha mjini kukaa rumande kwa zaidi ya miezi minne sasa pasipo kupatiwa dhamana kimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iwajibishwe

Katika mtandao wake wa kijamii Mh. Zitto amedai kuwa kitendo cha  Mbunge huyo ambaye ni muwakilishi wa wananchi kunyimwa dhamana  ni siasa za ukomoaji ambazo zinajenga chuki kwenye jamii na chuki huwa zinazaa visasi.

"Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP, Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi" Ameandika Zitto Kabwe

Hata hivyo kauli hiyo ya Zitto imekuja mapema leo baada ya  majaji watatu  kutoka mahakama ya rufaa kuitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na DPP kuwa makini na kuwataka kuwashikilia watu kwa misingi ya kisheria na kuongeza kuwa haipendezi na haingii akilini mtu  kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki ya dhamana.

"Mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua mpaka  mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushtua sana". Alisema Jaji Stella Mugasha.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zitto acha siasa, kisheria wewe ni layman, hivi mwenye mamlaka ya kutoa dhamana mahakamani ni DPP au mahakama? kimsingi baada ya pingamizi la DPP kuhusu dhamana, mahakama ilikuwa na nafasi ya kusikiliza hoja za pande zote kisha kupitisha uamuzi tokana na hoja hizo na sheria inavyotaka ndipo hutoa dhamana, upande usio ridhika na maamuzi hayo hukata rufaa endapo maamuzi hayo yanaweza kukatiwa rufaa. ilikuwaje akanyimwa dhamana? je DPP ndie anae toa dhamana mahakamani, sio mahakama? unaogopa kuiambia mahakama ilikosea? unahofu kunyooshwa? mbona hutaki kusema ukweli? kwa uelewa wangu wa sheria, mawakili wa Lema walikosea, badala ya kukata rufaa juu ya maamuzi ya mwanzo ya mahakama, wao wakaomba marejeo, wakapigwa chini na mahakama, kama walikuwa sahihi kwa nini mahakama iliwapiga chini? manake hiyo ni TKO(technical knock out) msitafute huruma, fuateni sheria mtaheshimiwa. Kumbuka hakuna alie juu ya sheria haijalishi wewe ni Mbunge au mkulima wa kule Kazuramimba Kigoma. Mtanyooka tu!Fiat Justitia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad