Zitto kabwe: Nimepata Kitu Juu ya Mahakama na Kesi ya Mbowe...!!!!


Nimetambua ( taken note ) uamuzi wa mahakama kuzuia amri ya kukamatwa ya mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA. 

Nimefurahi kuwa Mwanasheria wa Act Wazalendo ndg. Albert Msando ni mmoja wa jopo la wanasheria wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA ndg. Freeman Aikaeli Mbowe.

Mfumo wa Vyama vingi nchini upo hatarini, ni LAZIMA wana mageuzi wote kuweka tofauti pembeni na kupambana kulinda Demokrasia yetu. 

Tukiendekeza tofauti zetu ambazo nyengine ni za kijinga jinga tu, tutakuja shtuka hata hicho kinachotupa tofauti ( vyama ) hakipo.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Amkeni sasa. Imechukua muda mwingi kuiona hii. Acheni uchu wa madaraka kwanza. Muwaweke Watanzania na Tanzania mbele ya maslahi yenu binafsi. Mmeona jinsi awamu ya nne Mkuu wa nchi kutotumia kiti chake kuwachukulia hatua mafisadi wakuu nchini, na waleta madawa. Hawa wauzaji ni watu wadogo sana. Wasambazaji ni watimiza mujibu tu. Polisi wanalisti nzima ya watu walioshikwa phycically. Majina ya vigogo wasafirishaji kutumia meli zao. Mliwashika wakatoa vielelezo mkawaachia. Leo mnawaburuta watu kwa kulipa kisasi, Hii ni dhabi kubwa kwa Wakristo na Waislamu pia.Bandarini mlishika hivi vitu Polisi mnajua ,
    Je Mbona haya yote mmeyagubika. Mafisadi mmeyagubika. Sasa mmemweka Raisi Magufuli mwenye nia lakini mmeyakumbatia bado hayo majina , na polisi mnakwenda kuvurumusha watu waliosimama kidete nyuma ili kuwakingia vigogo, Je mtayatayuaje hayo? Watuhumiwa wanahukumu wapi fairness.Mnafunika volcano kwa kuwasha volcano dhaifu. Mnaogopa nini? mmmeikalia Katiba ambayo ilikuwa kunga ya Raisi itoke, yeye Raisi akaifunika. Nini lele mama. Wasomi wa nchi wanadharalika, wasio wasomi wanaendesha nchi vipi mtaendelea kwa kutoithamini elimu na kutokumthamini Mtanzania msomi. Badala yake Mnawaita Wachina, Wafaransa, Wajerumani, Wamarekani, Warusi wote hawa ni mabepari wakuu na wanaihujumu nchi sababu wanajua Viongozi wetu bado hawana mwanko wa kimataifa bado. Mgeni anachake kimoja, chukua ondoka.Mtanzania bado ananyanyasika nyumbani kwake, mnamfanya awe inferior kwa nini? Toka tupate uhuru miaka hamsini ni kubabaisha tu. Uzalendo haupo. AIBU viongozi wa chama Tawala kuunga mkono unyanyanyasaji na udharalishaji wa viongozi wetu. Unamfanya hata watoto mitaani wamdharau, Nini hiki. Pesa au maendeleo ya kweli na hadhi , heshima na utu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad