Alichokisema Nape Nnauye Baada ya Kuibuka kwa Account yake Feki ya Twitter Inayosambaza Habari za Kumpunda Magufuli..!!!


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameukanusha ujumbe unaotumwa kupitia akaunti ‘feki’ ya twitter yenye jina lake na kuwataka wanaofanya hivyo waache kwani anawafahamu na atawataja.

Nape ameandika hayo leo  sita mchana baada ya akaunti hiyo feki kuandika:

“Amemzuia Kinana kuzungumza, akae akijua hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”

Akaunti hiyo feki  pia iliandika:

“Siyo wote wenye nidhamu ya woga kunyamazia udhalimu unaowafanyia, utawazuia watu kuzungumza hadi lini? Katibu wangu piga moyo konde”

 Nape alikanusha na kuandika:

“Mnahangaika nini kunichafua kwenye twitter, hizi tweet zinazosambwa za maneno yasiyo na busara siyo zangu, nilishasema jana nikamaliza, nitawataja sasa!”

 Leo asubuhi Nape aliandika ujumbe wa kuwashukuru wanahabari na kusema alikuwa hajui kama wanampenda kiasi kile.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad