Kuna habari zilizoko chini ya viunga vya watawala zinasema watu wa ‘’kitengo’’ wameamua kulifanyia kazi suala la Mchungaji Gwajima, Clouds Media International na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa sababu halitoi afya njema kisiasa.
Kwa kifupi, ‘’kitengo’’ ni neno ambalo kwa kiingereza ni ‘’The ruling class/The Establishment’’. Hawa ni watu ambao moja ya kazi zao ni kutathmini kwa kina hali ya kisiasa, kiuchumi na kiulinzi nchini halafu baadaye hutoa mwelekeo kwa taasisi zinazohusika.
Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa hatutaweza kumsikia tena Mchungaji Gwajima akimzodoa Makonda katika mahubiri yake kanisani.
Ieleweke kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika, watu wa ‘’kitengo’’ walifanya tathmini na kubainisha watu ambayo wataweza kufanikisha mikakati ya kisiasa kwa CCM na kiuchumi kwa serikali katika mikoa ambayo inaonekana ni muhimu sana kisiasa na kiuchumi. Mikoa hiyo muhimu sana ilipelekewa viongozi ambao watafanikisha mikakati hiyo na mojawapo ni Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa wale wanadhani Makonda ataondolewa hivi karibuni katika Mkoa wa Dar es Salaam, nadhani wataendelea kusubiri sana mpaka pale watu wa ‘’kitengo’’ watakapo jiridhisha kuwa kazi waliyomtuma ameshindwa kuifanya au makosa anayofanya ni makubwa kiasi kwamba yanaondoa hata madhumuni makuu ya uwepo wake kama Mkuu wa Mkoa.
Nimalizie kwa kusema, Mkuu wa taasisi ya watu wenye ‘’suti nyeusi’’ ametoa onyo kali kwa vijana wake kwa yaliyotokea Clouds Media International na kwa Nape Nnauye kwa sababu kazi waliyopewa ni kumlinda Mkuu wa Mkoa na sio yeye Mkuu wa Mkoa awape kazi za kufanya nje ya misingi yao ya kazi. Ieleweke kuwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina kiulinzi ilibainika Makonda anatakiwa kuboreshewa ulinzi.
Msishangae sana kwa nini Nape Nnauye ameamua kuwa kimya kuhusiana na kadhia ya kutishiwa bastola. Ameelezwa ukweli wa hali halisi iliyopelekea kitendo hicho kutokea.
Mjumbe hauwawi! Naiwakilisha jinsi ilivyo!
Nchi ya ajabu hii. Usomi hauna faida.ukipendwa na raisi huna hsja ya elimu. Utakuwa kiongozi. Pia kula na wakubwa wakubebe.
ReplyDeleteHili bi bora na linahitajuka kwa wakati kama huu.
ReplyDelete