Askofu Achekelea Sadaka Kuongezeka Kanisani..!!!


Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (KKKT), Dayosisi ya Pare, Charles Mjema amewapongeza waumini wa usharika huo kwa kuongeza mapato yanayotokana na sadaka.

Askofu Mjema amesema hayo akiwa ni mgeni rasmi wa mkutano mkuu wa 20 wa Dayosisi ya Kaskazini uliofanyika kwenye dayosisi hiyo.

“Nimeona kwenye taarifa yenu hapa mwaka 1995 sadaka ilikuwa Sh9.4 milioni, lakini mwaka jana matoleo yenu kwa ajili ya kazi ya Bwana yamefikia Sh412.9 milioni. Hongereni,” amesema.

Askofu Mjema amesema wapo watu wanaoogopa kuweka malengo makubwa kwa kukosa ujasiri kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kumtolea Mwenyezi Mungu.

Awali, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Karanga wa mjini Moshi wa Dayosisi ya Kaskazini, Fred Njama amesema nchi imekumbwa na tatizo kubwa la ajira kwa vijana wanaomaliza elimu ya juu.

“Naishauri Serikali ione kwa jicho pana kwamba kwa kurundika vijana bila kujua mustakabali wao tunatengeneza bomu ambalo linasubiri kulipuka,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad