Ayaaah..Nape Azidi Kutoa Kauli Juu ya Ikulu,Safari Hii Amesema Haya Kuhusu Msemaji wa Magufuli....!!!


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa ubunifu wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano.

Nape ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kumwagiza mkurugenzi wa habari maelezo, kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kuona kama utendaji wao unaleta tija kwa jamii.

Akizungumza jana (Jumatano) Waziri Nape amesema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili maafisa mawasiliano wa Serikali, kurugenzi za mawaziliano Ikulu na idara ya habari maelezo wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali.

 “Nawapongeza wakurugenzi vijana, Dk Hassan Abbasi (Maelezo) na Grayson Msigwa wa Ikulu.  Hawa ni mfano wa ubunifu  wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Serikali yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa,”amesema Nape.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad