Baada ya Umoja wa Mataifa Kutangaza Kuingilia Sakata la Kupotea kwa Ben Saanane,Chadema Waibuka na Kutoa Tamko Hili Zito..!!!!


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Serikali kupitia vyombo vyake vya Dola kutoa sababu za kufuta jalada la uchunguzi wa Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa chama hicho, Ben Saanane ambaye ametoweka tangu Novemba mwaka jana.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alisema jana kwamba jeshi hilo linafanya kazi yake huku akihoji, “Chadema wamejuaje kama hilo jalada la kesi ya Saanane limefutwa?

“Nenda kawaulize tena, wao wamejuaje, wakueleze vizuri hilo jalada limefutwa vipi na nani?”

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ilisema wanashangazwa na hatua iliyofikiwa na vyombo vya dola kufuta jalada la uchunguzi wakati kada huyo bado hajapatikana mpaka sasa.

“Tunajua DCI (Robert) Boaz alisema hawako naye lakini tunashangazwa na hatua yao ya kufuta jalada la uchunguzi mapema bila hatua nyingine,” inasomeka taarifa hiyo.

Hivi karibuni, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN) yenye makao yake makuu jijini Geneva, Uswisi, ilisema iko tayari kutuma timu ya uchunguzi.

Chadema imerejea kauli yake ya kuitaka Serikali kutoa maelezo ya wapi alipo Saanane iwe ndani au nje ya nchi kwani ndiyo yenye udhibiti wa mipaka yote majini, nchi kavu na angani.

Makene alisema Serikali ina teknolojia ya mawasiliano ya kuweza kujua na kupata mawasiliano ya mwisho ya mtu aliyewasiliana na kada huyo, wakati gani na juu ya suala gani.

Makene alisema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imeshindwa kufanya kazi yake na kumaliza tofauti na sintofahamu zinazoendelea.

Alisema ni aibu kwani taasisi za kimataifa zinaguswa na suala hilo huku vyombo vya usalama nchini vikikaa kimya.

Saanane, ambaye pia ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alipotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 18 mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad