Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Lasislaus Matindi amesema wamefanikiwa kukusanya shilingi Bilioni 9 kwa miezi minne tu kwa kutumia ndege hmbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Kipindi ndege hizo zinanunuliwa baadhi ya watu walikosoa kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC). katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC.
Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena serikalini kwa asilimia 100.