Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumuachia huru Rapa Emmanue Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kukamatwa juzi wilayani Mvomero mkoani Morogoro kisha kusafirishwa jana kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa kile kilichoelezwa kuwa wimbo wake wa WAPO alioutoa hivi karibuni hauna maadili na una maneno ya kichochezi.
Akitoa agizo la Rais Magufuli, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Rais Magufuli ametaka Nay aachiwe huru na wimbo wake aufanyie maboresho kwa kuongelea pia kuhusu wauza madawa ya kulevya na wakwepa kodi kisha uendelee kupigwa kwenye vyombo vya habari.
Aidha amesema kuwa, mara tu atakapoachiwa huru, Nay anapaswa kuonana na Waziri Mwakyembe ili ampe maelekezo yaliyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wimbo huo.
Kuna mtu alishtaki? Hili la Ney limefanyiwa kazi wakati lipo kwenye mitandao ya kijamii, Je la mkulu wa kanda maalum vp?
ReplyDeleteHahahah! Sio ki-hivo bana, unawanyima ulaji sasa akina Kibatala na Tundu Lisu, walishajipanga kupata ajira.....NDIO ZAO HIZO!!
ReplyDeleteILA HAWA WSANII WAJIFUNZE NYIMBO ZA KUIMBA WAACHE KUIGAIGA MAMBO YASIYOFAA NA KUTAFUTA KIKI AMBAZO UTAZIJUTIA BAADAE. OHOOOO!
ReplyDeleteHivi muheshimiwa kausikiliza vizuri huu wimbo kweli?? Ama kavutiwa na pale aliposema watu wanapenda udaku wa kwenye mitandao kuliko kazi..........maana humo ndani mpaka matusi YAMO....., nyimbo za Ney nyingi ni MATUSI MATUPU...khaaa!! Anyway, ANGURUMAPO-SIMBA-MCHEZA-NANI?
ReplyDelete