Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho kina mpango wa kufungua Chuo Kikuu cha chama hicho.
Akizungumza katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na Channel Ten ambapo amesema chuo hicho kitatoa mafunzo kwa wanachama, makada na viongozi wote wa chama na hata waliopo serikalini kupitia chama ili kuwafundisha itikadi za chama hicho.
Alisema, “Unajua chama cha Mapinduzi na chama cha kikominist (Uchina) ni marafiki, tumeamua tujenge chuo kikuu cha chama cha mapinduzi ambacho kitakuwa na kazi ya kuwafundisha wanachama, makada,viongozi na wale waliopata dhamana serikalini. Kupitia chama cha mapinduzi tutawafundisha ili tuelewane itikadi yetu, watu hujiunga na chama si kwa ajili ya ushabiki ila watu wanajiunga na chama kwa sababu wanaamini wameielewa itikadi ya chama hiki ni nini.”