Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mkutano wake Mkuu maalum wa Taifa Machi 12 mwaka huu lengo likiwa ni kufanya marekebisho ya kanuni na katiba ya chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo amesema kuwa pamoja na mambo mengine mkutano huo pia utafanya kazi ya kujadili na kupitisha marekebisho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2012 pamoja na kanuni za chama hicho na jumuiya zake.
Amesema pia mkutano huo utapokea taarifa ya ratiba ya uchaguzi Mkuu wa CCM na jumuiya zake utakaofanyika nchini kote mwaka huu wa 2017.