Diamond Aipiga Dongo Serikali,Atoa Yake ya Moyoni...!!!


Diamond Platnumz akihojiwa kwenye kipindi cha Clouds 360, ameulizwa swali kuhusu wasanii kutangaza utalii wa Tanzania. Katika majibu yake amesema kuwa serikali imeshindwa kuwekeza pesa kwa wasanii ili kutangaza utalii na badala yake wanapoteza pesa nyingi kwa taasisi za nje.

Amesema kuwa kwa South Africa kupitia board yao ya utalii wana utaratibu mzuri na wamewekeza kuhakikisha utalii wao unatangazwa na ndio maana hata yeye ametumiwa kuutangaza utalii wa South Africa.

Amesema kwa hapa Tanzania alishawahi ku-apply TANAPA ili kuvitangaza vivutio vya kitalii Tanzania lakini mwisho wa siku akapigwa danadana na kuambiwa yeye inabidi ajitolee kuwa Goodwill Ambassador, sasa unakuwaje goodwill ambassador wakati unatakiwa kuwekeza kwenye kutangaza vivutio!! Unahitaji salio kwenye simu, nauli nk!!

Anasema serikali haioni thamani ya Mtanzania kabisa, wakati wasanii wana wafuasi wengi wa ndani na kimataifa kwenye mitandao ya kijamii ambayo wangeitumia kutangaza utalii.

Pia amesema suala la ku-shoot video Tanzania kuna vikwazo vingi sana kama kupata maeneo na nyenzo nyingine. Hivyo wasanii kutumia gharama kubwa kutangaza vivutio vya South Africa kwenye video zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad