Duh..Straika wa Zanaco Aliyefunga Goli la Kusawazisha Ametoa Kauli Hii Kuhusu Simba...!!!!


STRAIKA wa Zanaco ya Zambia, Kwame Attrams, raia wa Ghana, amesema anatamani siku moja kuja kukipiga Simba.

Attrams ndiye aliyeisawazishia Zanaco baada ya Yanga kutangulia kufunga  wakati walipotoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na juzi, Attrams alisema akizichezea Simba inaweza kuwa njia ya kwenda kusakata kabumbu Ulaya.

Attrams alisema lakini atakuwa tayari kuichezea Simba kwa kuwa ni timu kongwe na zinafuatiliwa na mashabiki wengi barani Afrika ikiwamo nchini Ghana.

Straika huyo aliyezichezea timu za Groupe Spotive Bazano ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Wadi Degla ya Misri, alisema malengo yake ni kutaka kuona siku moja anacheza soka Tanzania katika klabu hizo mbili zenye historia kubwa.

“Simba na Yanga ni timu kubwa,  nimeanza kuzisikia tangu nikiwa mdogo natamani siku moja na mimi nije Tanzania kufanya kazi na moja ya klabu hizi,” alisema Attrams.

Alisema anajisikia furaha kuifunga Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na tayari ameingia katika historia ya kuwatungua Wanajangwani hao.

Attrams alisema atajisikia zaidi akicheza pamoja na Waghana wenzake wanaokipiga Simba, James Kotei na Daniel Agyei.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad