Ehe..Umesikia Alichosema Mwakyembe Juu ya Wizara Yake..?


Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema tangu aingie katika wizara hiyo, wameboresha mazingira ya kisheria na ya mahakama.

Akizungumzia mjini Morogoro katika ziara ya siku mbili, pia ametoa wito kwa wananchi kuwaripoti mahakimu wanaokwenda kinyume kwenye kamati za maadili ambazo zimeundwa kila wilaya zikiwa chini ya wakuu wa wilaya ambao ni wenyeviti na makatibu tawala wa wilaya ni makatibu.

“Mkiwaona mahakimu ama kwa vitendo vyao, mwenendo, matamshi au wanakiuka kutenda haki, muwaripoti katika kamati hizi ambazo zina nguvu na zimeundwa maalumu kupunguza malalamiko ya wananchi. Uamuzi wa kamati hizi unakwenda hadi Tume ya Utumishi ya Mahakama,” amesema.

Akizungumzia biashara ya fedha, amewaonya wananchi kutojihusisha na kukopesha fedha bila kuwa na kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kuwa ni kujihusisha na biashara haramu jambo ambalo halitavumiliwa.

Awali, Dk Mwakyembe amesema kuanzia mwezi Mei hakutakuwa na ndoa itakayofungwa nchini bila wahusika kuwa na vyeti vya kuzaliwa, lengo likiwa ni ili Taifa liweke vizuri kumbukumbu za raia wake.

Amewataka watu waliotajwa kisheria kuwa wanaweza kufungisha ndoa, wajiandae kutekeleza agizo hilo na kwamba uamuzi huo utakuwa ni wa lazima kwa kila mwananchi
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad