Ngono si desturi ya kila siku hata kwa wapenzi walio mabingwa kitandani. Hata hivyo, kukosa kushiriki ngono kwa muda mrefu kuna madhara yake ambayo watu wengi hawayafahamu.
Utafiti uliofanywa na British Association for Sexual Health and HIV ulibaini madhara haya yaliyowakumba wapenzi wengi:
Mafadhaiko na wasiwasi mwingi
Kushiriki mapenzi kutakuletea raha sasa hivi na siku nzima.
Homoni ya endorphins ambayo hutolewa wakati na baada ya kulishana mahaba husaidia kukuchangamsha na hivyo kukuondolea mawazo. Ukizima mapenzi hutanufaika na kitulizo hiki.
Mwanamume anajinyima fursa ya kumzuia kupatwa na kansa ya tezi
Imebainika kuwa wanaume ambao huacha kufanya ngono hukosa manufaa ya ziada ya ulinzi dhidi ya kansa ya tezi.
Utafiti uliowasilishwa kwa shirika la American Urological Association ulipata kuwa wanaume ambao hushiriki mapenzi zaidi hujipunguzia hatari ya kupatwa na maradhi hayo kwa asilimia 20.
Sababu kuu ni kuwa shughuli ya kufyatua mzinga mara kwa mara yaweza kutupa nje vitu hatari kutoka kwa tezi hiyo.
Utaishi kutoa kamasi na kulalamika homa
Watafiti pia wamethibitisha kuwa shughuli nzima ya kusakata ngoma huimarisha kinga ya mwili.
Watu ambao hushiriki mapenzi mara moja ama mbili kwa wiki huimarisha kinga yao ya immunoglobulin A kwa asilimia 30 ikilinganishwa na wale ambao hula mahaba mara chache ama hukosa kabisa.
Kudidimia kwa udhibiti wa kibofu na nguvu za kiume
Ngono pia hukusaidia kufanyisha zoezi misuli ya kibofu na kukuondolea matatizo ya nguvu za kiume. Unavyozidi kushiriki mapenzi ndivyo unazidi kuimarisha fursa ya mzinga kusisimka.
Kiwango cha mafadhaiko huongezeka
Utafiti umethibitisha kuwa ukishiriki ngono mara kwa mara huwezi kukumbwa na mawazo kwa sababu kuna ongezeko la homoni zinazohusika kukuletea uchangamfu. Ngono hukusaidia kudhibidi mafadhaiko yanayokukumba.
Ndoto zako hubadilika
Ukikosa mapenzi utaanza kuota ukishiriki ngono ama hata kushikwa na nyege usingizini. Tatizo ni kuwa hii ni ndoto tu!
Ubongo huduwaa
Wanasayansi wamebaini kuwa tendo la ngono huimarisha ukuaji wa neva katika eneo la ubongo linalohusika na shughuli ya kudumisha kumbukumbu, hippocampus.
Kama tujuavyo kumbukumbu nzuri ni kifaa muhimu masomoni kwani itakuwezesha kuyakumbuka mambo uliyofunzwa darasani ama kusoma vitabuni, na hiyo itakuweka pazuri wakati wa mtihani.
Kisima cha mwanamke hulegea
Ngono ni zoezi mwafaka kwa kisima chako. Shughuli ya misuli kujikunyata na kuachilia huchangia kubana kisima.
Kwa upande mwingine, ukosefu wa ngono hufanya misuli hiyo kulegea na kisima kuwa legevu.