Gwajima Azidi Kumfukunyua Makonda,Ataja Makosa ya Kisheria Yaliyomfanya Akimbie Nchi na Adhabu Anazostaili Kupata...!!!,


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.


Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.


“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema


Gwajima alisema kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki ni kifungo cha miaka mitatu.


Kosa jingine alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Gwajima ni mwanasheria au muhubiri. Watu wanakuja kanisani kusikia mahubiri au siasa uchwara??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ni BASHITE nini? UTAISOMA NAMBA.. HAPA VYETI TU

      Delete
  2. Jamani basiiiiii inatosha sharia zipo muacheni

    ReplyDelete
  3. HUYU MPIGA DEAL TU,HANA CHAUCHUNGAJI WALA NINI..NA HAO WAUMINI WAKE MANDONDO YANAMUITIKIA TU ..

    ReplyDelete
  4. Gwajima hata wewe tunajua mengi ya kwako ila tunakustahi,mwache sasa Makonda tafadhali.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad