Haya Hapa Maneno Aliyosema Paul Makonda Baada ya Kutimiza Mwaka Mmoja Kama Mkuu wa Mkoa


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Machi 15, 2017 anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Machi 13, 2016 na kuapishwa Machi 15, 2016.


==>Haya ni Baadhi ya Maneno Yake


1.Namshukuru Rais Magufuli kwa kusikiliza kauli ya Mungu na kunikabidhi mamlaka ktk mkoa huu wa Dar.


2.Navishukuru sana Vyombo vya Habari kwa kuwa daraja kati ya Serikali ya Mkoa na wananchi. Wamefanya kazi kubwa!


3.Nawashukuru sana vijana tuliowakamata wa mwanzo(TID na wenzake), wamekuwa mfano mzuri kwa wenzao na Mungu awasaidie


4.Mwaka wangu wa II nikiwa kama RC wa Dar, kasi itaongezeka maana nimekomaa sasa. Nitahakikisha jiji linarudi kwny mstari.


5.Kuna makampuni ya barabara mawili nimeshayapiga marufuku kwa sababu ya kujenga barabara chini ya viwango.


6.Katika vitu nimeweka msingi mzuri ni kinondoni, kesi za ardhi zinasikilizwa mpaka jumamosi


7.Kazi hii nimepewa na Mungu, acha idadi ya wanaomchukia Makonda waongezeka lakini niwe na uhakika na Mungu wangu


8.Tumeamua kufanya vitu hadharani kwa sababu hatutaki kupokea rushwa wala fedha haramu


9.Hatuna kisasi na mtu, ndio maana upande huo wanapigana sisi tunacheka


10.Kupitia fedha za dawa za kulevya, watu wamejenga maghorofa yanakwenda kwa kasi sana na wamefanya hata thamani ya viwanja ipande


11.Fedha hizi za dawa za kulevya zinaenda kukauka DSM ili kila mtu ale kwa jasho lake


12.Tutaanza mfumo wa kutumia kadi ili tukusanye kodi yetu na kila mtu ale kwa jasho lake, kuna watu wanaficha fedha


13.Kipindi hiki ni cha kazi. Nawapongeza wote wanaofanya kazi kwa bidii na kuifanya Serikali isimame kidete


14.Changamoto mojawapo niliyokutana nayo ni MUDA! Muda hautoshi, nahitaji hata miaka kadhaa ili kumsikiliza kila mwananchi


15.Changamoto nyingine ni mazoea ya Watendaji wa Serikali ktk kutoa huduma. "Njoo kesho" imekuwa kero kwangu na kwa wananchi


16.Kuzungushwa kwa wananchi kunapelekea changamoto katika za Serikali za Mitaa kuletwa ofisini kwangu. Hili nalo ni tatizo!


17.Nampongeza sana Kamishna Sirro na Awadhi (wa Usalama barabarani) kwa kusimamia ulinzi na usalama jijini Dar


18.Milio ya risasi ilikuwa kawaida Dar, watu waliogopa hata kwenda Mlimani City kwa hofu ya kuporwa. Tumeyakomesha yote hayo


19.Mtu anataka nikae kimya wakati wananchi wangu Dar wanateseka kwa matumizi ya DawazaKulevya... Nauliza "Wewe ni NANI?"


20.Tunapambana kupigania ndoto za vijana na matumaini ya wazazi wao. Haijalishi tumechelewa kiasi gani lakini hatutoacha!


21.Wapiga dili wa Bandarini jijini Dar wamekuwa wakisumbua kwa fedha zisizo halali na kuwasumbua wafanyabiashara halali


22.Sibabaishwi na watu wanaonichukia wakati nikitekeleza majukumu niliyopangiwa na Rais Magufuli kama Mkuu wa Mkoa.


23.Bureau de Change zinatumika kufichia pesa haramu. Wiki ijayo moto utawaka, lazima tushughulikie maficho haya.


24.Sasa foleni jijini Dar imepunguzwa kwa kiwango kikubwa na askari. Ukifurahishwa na trafiki toa shukrani zako, tuwape moyo.


25.Mwaka huu wa pili tutakazia sana kwenye utumishi. Nitaanzia kwenye Serikali za Mitaa nione jinsi wanavyowasaidia wananchi.


26.Nataka mwananchi apate majibu kamili aendapo Ofisi ya Umma. Kama hawawezi kumsaidia waende wao ofisi ya juu sio mwananchi.


27.Wanaoishi mabondeni jijini Dar na wana hati halali nitawapa viwanja. Watendaji waliotoa hizo hati nitawashughulikia!


28.Najua wengi wanaoishi mabondeni wamepangishwa na waliolipwa fidia. Huwezi kuwa na akili timamu ukakubali kupanga bondeni


29.Hivi karibuni nitaelekeza wapi showroom za magari zinatakiwa ziwe jijini Dar. Nataka magari yote yauzwe eneo moja


30.Ninawashukuru wanasheria wetu 35 wanaotoa msaada na ushauri wa kisheria bure kwa wananchi wa jiji la Dar wasio na uwezo


31.Tumepewa eneo kubwa la kujenga kambi kwa ajili ya wahanga wa DawazaKulevya. Hii itatusaidia kufuatilia mienendo yao


32.Hadi sasa tuna watu 11,854 jijini Dar waliokubali kuacha matumizi ya DawaZaKulevya kwa hiari. Haya ni mafanikio makubwa


33.Wengine tukiwaita Kituo cha Polisi wanatumia Colgate na Chumvi ili wasigundulike ktk vipimo. Tuna mbinu mpya za kuwapima


34.Kuna wanaowatumia watoto wadogo kufanya uhalifu na kabla ya hapo wanawavutisha bangi. Tunawasaka na tutawakamata!
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Good job Makonda wenye wivu na wewe wajinyonge.

    ReplyDelete
  2. Nampenda huyu kaka mpaka natokwa na 'vipele vya baridi', kwasababu ana-hofu-ya-Mungu, ana-jitambua, ana-jikubali, ana-jiamini, ana-chapakazi, ana-jali-muda, hana-longolongo, hana-roho-mbaya, ana-huruma-sana, na kubwa kuliko yote, HAOGOPI-DUDU-WALA-MENDE!! Naomba Mungu azidi kumlinda, hao maadui zake washindwe na walegee..........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad