1. Magonjwa ya "Urinary tract infection" au UTI hayataisha kwako. Hii hasa ni kwa wanawake wanavaa nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu zaidi ya saa kumi. Unavaa chupi, lakini tight, suruali ya jeans, nk halafu unashinda na hizo nguo kuanzia asubuhi unapoenda kazini hadi saa mbili usiku unaporudi home. Hiyo ni hatari sana. Mwanamke anayefanya kazi zinazompasa kuwepo kazini zaidi ya masaa 8 namshauri asiwe anavaa chupi kabisa. Chupi ivaliwe nyakati za hedhi tu.
Kama hauko kwenye siku zako vaa suruali tu bila chupi. Au vaa underskirt pekee yake kwa ndani na ndoo uvae nguo yako ya kawaida.
Hii itakuepusha na kuugua UTI. Ukiacha sababu za ngono UTI husababishwa na bacteria wanaopendelea mahali penye unyevu na joto. Kwa hiyo mwanamke akivaa nguo nyingi bacteria hao hujipatia joto la kutosha kuzaana. Mwanamke ni vyema ukaepuka kuvaa nguo za kubana mwili sana ili kuepukana na uwezekano wa kupafanya ukeni pawe na joto sana na ikitokea bacteria mmoja tu akaingia humo atazaa haraka sana na kujikuta UTI inakuwa rafiki yako. Vaa sketi bila chupi au kama kuvaa suruali ni lazima hakikisha unavaa suruali peke yake. Jizoeze tu utazoea. Na ukizoea kuvaa nguo bila chupi utainjoi sana.
2. Magonjwa ya kuvu au fungus hayatakoma kwako. Bado niko kwa wanawake, kama nilivyoeleza mwanzo hapo magonjwa ya fungus yanasababishwa pia na kuvaa chupi kwa muda mrefu. Chupi inayovaliwa kwa zaidi ya saa 8 lazima italeta ukungu au uvundo sehemu nyeti. Huo uvundo waweza kuleta fungus ukeni. Fungus za ukeni hazina tofauti na zile za miguuni kwa wanaume wanaovaa viatu kwa muda mrefu bila usafi miguuni wa kutosha. Chupi inakuwa kama socks za wanaume. Mwanamke avaae chupi muda mrefu bila kuruhusu upepo upite ndani ni watapata fungus ukeni sawa na mwanaume anayevaa socksi zisizofaa kiafya.
Chupi au socks zinazofaa ni zile za pamba au cotton. Of course sababu za kupata ugonjwa wa fungus kwa mwanamke siyo tu kuvaa chupi inayobanaaaa kwa muda mrefu ni pamoja na kutawadha kwa kutumia maji. Wanawake wengi hawajui kutawadha kwa kutumia maji.