Hii Ndio Sababu ya Darassa Kupiga Chini Show ya Nairobi Jumamosi iliyopita!

Darassa yuko nchini Kenya kwa ziara ya kimuziki na alitarajiwa kupiga show ya kukata na shoka Jijini Nairobi Jumamosi iliyopita, March 18. Licha ya mashabiki wake nchini Kenya kuwa tayari kukata kiu kutokana na burudani kutoka kwake, Darassa hakufika wala kupanda jukwaani. Kwanini?

Kutokana na kukosekana kwa staa huyo wa Muziki kwenye show hiyo, mtangazaji wa radio Citizen Mzazi Willy M Tuva alimualika Darassa kwenye kipindi cha Mambo Mseto ili kuelezea ni kwanini aliipiga chini show hiyo. Na pia katika mkutadha huo, Tuva alichukua fursa hiyo kufikia watayaarishaji ama waandaji wa show hiyo ili kubaini chanzo halisi cha kufeli kwa show hiyo ambayo ilitarajiwa na wengi.

Je tatizo lilikuwa ni nini mpka Darassa hakuweza kutoa burudani kupitia show hiyo? Darasaa anasema kupitia kituo cha radio Citizen alishukuru wa Kenya kwa support. Halafu alifunguka kuwa waandaji wa show walimfuata nyumbani Tanzania ambayo ilikuwa jambo la busara.

Lakini waandaji walienda nje ya mkataba kwa kukurupuka kupanga show ambayo ilikuwa nyuma na ratiba yake. Maana walipanga show wakati yeye hakuwa amelipwa, na walikuwa wamekubaliana kuwa waandaji wa show hiyo wangelipa kwanza halafu ndio wafanye matangazo. Lakini hawakufanya hivyo ila walifanya matangazo kwanza halafu baadaye ndio wakampigia simu Darassa aje apige show halafu ndio alipwe hivyo ikapelekea Darassa kuipiga chini show hiyo.

Kwa upande mwingine msemaji wa waandaji wa show hiyo, Martin, alisema kuwa kitu kilichofanya show hiyo kufeli ni wakati ulikuwa mfupi. Hata hivyo Venue(KICC) ambayo ilikuwa imechaguliwa ilikuwa na tight schedule lakini hata hivyo walikuwa wameipata, lakini mawasiliano kati yao na Darassa hayakuwa mazuri kufikia siku ya show.

Kwa hivi sasa jina Darassa limekuwa ni brand inayopendwa sana nchini Kenya, kila mahali ngoma yake ya Muziki imekuwa ikipasua anga za sehemu zote Kenya. Si sehemu za burudani, redioni, kwenye runinga, sokoni, kwenye magari(Daladala).

Ngoma hii imekuwa inagusa na kupendwa na watu wa kila rika. Hivyo inazidi kumpa Darassa fursa ya kung’ara zaidi na kutamba si Kenya tu bali ndani na nje ya Afrika Mashariki. Nairobi inakuwa kitovu cha burudani, na msanii yeyote anapokubalika katika jiji hili basi ajue ana nafasi ya kuiteka Afrika kwa ujumla
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad