Historia ya Paul Makonda Iwasisimue Vijana Wanaokutana na Changamoto Katika Maisha


Rai yangu, Historia ya Paul Makonda Iwasisimue (inspire)Vijana wanapokutana na changamoto kwenye maisha na kujifunza namna ya kushinda.

Juzi hivi nilipata kumsikiliza Mh Paul Makonda akielezea historia ya maisha yake iliyojaa changamoto nyingi. Clip hiyo ikanikumbusha maneno aliyoniambia Paul Makonda mwaka 2009 wakati tunakwenda Dodoma. Alivyoeleza kwenye clip ndivyo alivyonisimulia siku ile tukiwa safarini kwenda Dodoma. Siku ile alipokuwa akinisimulia aliishia kulia kwa uchungu. Pia niliumia sana.

Alipokuwa akinisimulia, mara kwa mara Paul Makonda alisema "lakini sikukata tamaa niliendelea kumtumaini Mungu". Hakukata tamaa na ndiyo sababu ya yeye kufika alipofika.

Kuna picha inaonyeshwa na kudaiwa hapo ndipo alipozaliwa. Sehemu duni. Kuna picha zinaonyeshwa Paul akiwa kwenye mazingira duni, kuna picha zinamwonyesha akilia, lengo ni kumdhalilisha.
Rejeeni historia za watu maarufu duniani leo, wengi walikuwa watu wa kawaida na huenda duni lakini walikabiliana na changamoto bila kukata tamaa na wakashinda. Mmoja ni Baraka Obama.

Obama kwao ni Kenya. Na alipokuwa anagombea mara ya kwanza republicans walitoa picha ya Obama akiwa na bibi yake kijijini kwenye nyumba duni, lengo wamdhalilishe. Obama hakukata tamaa na hatimae akawa rais wa Marekani ambayo yalikuwa makusudi ya Mungu.

Hakuna binaadam amayepanga azaliwe wapi na wazazi wapi. Watu wengi, kwa kukabiliana na changamoto katika maisha hufanikiwa kubadili maisha yao na kufikia mafanikio makubwa, hasa kwa kutokata tamaa na kumtumaini Mungu. Vijana nilidhani mngejifunza hilo kwa Paul Makonda badala ya kukejeli.

Kingine ambacho nimeona nikiandike, mimi ukweli nashangaa kuona wengi wanaomdhihaki Paul Makonda siyo wapagani. Ni watu wenye dini, tena dini maarufu. Inasikitisha sana.

Kuwa na dini na kumjua Mungu ni vitu viwili tofauti. Unaweza kuwa kiongozi wa dini lakini humjui Mungu wa Kweli. Tabia moja kuu ya Mungu ni upendo. Mungu ni pendo. Pendo huvumilia, hustahimili, nk. Hivyo, tabia hii inatakiwa kudhihirika kwa watumishi wa Mungu.

Yesu Kristo alimfunua au alidhihiridha upendo wa Mungu alipokuwa msalabani akiteseka ili aukomboe ulimwengu. Akiwa msalabani alisamehe, hakulaani. Alipnyesha upendo wa Mungu. Alipotukana na kudhihakiwa hakurudidha mashambulizi bali alibariki. Aliposingiziwa, hakuwatisha waliomsingizia bali aliwaombea. Yesu Kristo alitoa pepo na kuyaelekeza apepo yaende kwa nguruwe, hakuyapeleka kwa binaadamu aliokuja kuwaokoa.

Lakini hali inavyoonekana sasa inasikitisha. Hilo nalo tujifunze.

Vijana wengi wanaangamia kwa kutumia madawa ya kulevya. Bila hatua madhubuti kuchukiliwa, ninahofu inawezekana Tanzania ikatawaliwa tena. Tena kirahisi tu. Hapatakuwa na rasilimali watu wenye kuwajibika na kulilinda Taifa hili.

Paul Makonda kathubutu, vijana na watanzania kwa ujumla, tuache itikadi ya vyama vya siasa tuunge mkono juhudi za kupiga vita madawa ya kulevya kwani madawa ya kulevya yanalingamiza taifa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad