Hivi Ndivyo Ahadi ya Rais Magufuli Ilivyotekelezwa kwa Spidi ya Kimondo..!!!


Ahadi ya Rais Dk.John Pombe Magufuli ya kutatua kero ya maji kwa wakazi zaidi ya 12,000 wa mji mdogo wa Kisesa wilaya ya Magu mkoani Mwanza,hatimaye imetekelezeka ndani ya miezi miwili, baada ya mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira jijini Mwanza ( MWAUWASA ) kutumia zaidi ya shilingi milioni 62 kujenga mradi wa maji katika mji huo na hivyo kumaliza kabisa kero ya maji ya muda mrefu.

Ujenzi wa mradi mpya wa maji Kisesa ulianza Januari 29 mwaka huu,siku 18 baada ya Rais john Magufuli, aliyekuwa akipita eneo la Kisesa akitokea Chato kuelekea Bariadi mkoani Simiyu kuombwa na wakazi wa mji huo awasaidie kutatua kero ya maji, ambapo alimuagiza Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi gerson Lwenge kuhakikisha anashirikiana na mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira jijini mwanza ( MWAUWASA ) kutatua changamoto hiyo iliyokuwa inawakabili wakazi wa kisesa.

Mkuu wa wilaya ya Magu Bi.Hadija Nyembo akizindua mradi huo amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kuihujumu MWAUWASA kwa kujiunganishia maji bila kufuata taratibu,sambamba na wanaojihusisha na wizi wa dira za maji na wanaoiba maji baada ya kusitishiwa huduma hiyo kutokana na madeni.

Baadhi ya wakazi wa eneo la Kisesa,wanaeleza jinsi walivyokuwa wakitaabika kwa kukosa majisafi na salama kabla ya mradi huo kukamilika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad