Hivyi Ndivyo Magufuli Alivyowahenyesha Vilivyo Wajumbe Wavivu na Wachelewaji Kwenye Mkutano wa Nec wa CCM..!!!


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (ccm), Rais John Magufuli, aliwahenyesha vilivyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) waliozoea kuchelewa ukumbini baada ya kufika mapema kadri ya ratiba na kuwaacha wengi wao wakihaha kwa takribani dakika 20 ili kuwahi viti vyao.

Awali, wakati alipoingia ukumbini, Magufuli alikuta wajumbe wasiozidi 20 na hivyo akalazimika kuwasubiri wengine kwa takribani dakika za idadi hiyo ya wajumbe (20) ili wengine wapate nafasi ya kuwamo.

Mara zote, baadhi ya wajumbe huchelewa kuingia ukumbini kutokana na mazoea kuwa mwenyekiti atachelewa, hata kama ratiba inaonyesha wazi kuwa anapaswa kuwamo ukumbini muda fulani.

Kwa sababu hiyo, wakati Maghufuli akiingia ukumbini, wajumbe waliokuwamo walilazimika kutoka nje na kuanza kuwaita wenzao kuwajulisha kuwa mwenyekiti alishaingia ukumbini kwa wakati.

Miongoni mwa wajumbe waliokuwamo ukumbini wakati Magufuli akiingia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, William Lukuvi; Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake (UWT), Amina Makilagi na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole.

Baada ya wajumbe kuingia, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema kikao hicho kina kazi moja kubwa ambayo waliianza tangu Desemba mwaka jana.

“Wajumbe waliopo baada ya wengine kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali za serikali, ni 382 na waliohudhuria kikao hiki ni 376,” alisema Kinana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad