Ikikumbukwe wakati anamkabidhi mwenyekiti Magu, Kikwete aliitaja changamoto kubwa inayokikabili chama kuwa ni wanachama kutolipa ada.
Leo katika hotuba yake ameonekana kushangazwa na sababu walizotoa Mwenyekiti na Katibu wake Kinana na kuiacha sababu kubwa na ya msingi wa mabadiliko waliyopendekeza . Ndiyo maana mwanzo amesema "wamekuwa wastaarabu kidogo" !! wameacha sababu ya msingi ya Ukata katika chama.
Suluhisho walilochukua la kukabili tatizo hili na kujificha nyuma eti kuleta ufanisi, limeonekana kumkera Kikwete.
Badala ya kutafuta mbinu ya kuwashawishi wanachama kulipa Ada, wameamua kuwapiga panga wajumbe ili wabaki wachache watakaoweza kulipana posho. Badala ya kutafuta vyanzo vya mapato ili kuweza kugharimia mikutano wameamua kupunguza mikutano na kusema eti wanalenga ufanisi.
Mbinu hii inaonekana kutumiwa Sana na mtawala huyu katika utawala wake: tujiuliza ni wafanyakazi wangapi walikuwa hewa wameondolewa na wangapi walioajiriwa ili hewa isiwe hewa bali wafanyakazi halali.