Watumiaji wa umeme nchini watakosa huduma ya ununuzi wa nishati hiyo kwa njia ya LUKU kwa takriban saa 12, kutokana na kuzimwa kwa mfumo unaohusika na huduma hiyo.
Taarifa iliyotolea na Shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) imesema kuwa mfumo huo utazimwa kuanzia siku ya Jumapili Machi 19 saa 4 usiku hadi siku ya Jumatatu saa 3 Asubuhi.
“Lengo ni kuboresha Mfumu wa LUKU katika uhifadhi wa wateja (Database). Tunaamini maboresho haya yatasaidia ufanisi katika manunuzi ya umeme” Imesema taarifa hiyo iliyotolewa jana na kitengo cha mahusiano cha TANESCO.
Aidha, shirika hilo limewataka watumiaji kufanya manunuzi kabla ya saa 4 usiku siku ya Jumapili na kuomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.