Humphery Polepole Afunguka Haya Juu ya Kinana...!!


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Humphery Polepole jana amefunguka na kuweka wazi juu ya hali ya Katibu Mkuu wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana na kusema kuwa kiongozi huyo kwa sasa hayupo nchini. 

Humphery Polepole akiongea na waandisha wa habari jana Makao Makuu ya Chama hicho Lumumba amedai kuwa Katibu Mkuu wa CCM amekwenda nje kwa matibabu 

"Katibu Mkuu wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana yuko nje ya nchi kwa matibabu na kuangalia Afya yake na anaendelea vyema"- Alisisitiza Humphery Polepole 

Mbali na hilo Polepole amedai kuwa CCM ni chama cha mfano kwa kurithisha maarifa kutoka kwa wazee na kuwafikishia vijana na kujenga msingi wa kuwa viongozi bora.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad