Huu ndio ujumbe wa Naibu Spika kwa taifa kuhusu wasichana
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Mwansasu ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kuongea na vijana wa kike ikiwa ni pamoja na kuwaweka wazi juu ya njia mbalimbali za kujisitiri pindi wanapoanza kuona mabadiliko katika miili yao.
Leo katika kipindi cha East Africa Breakfast, wakati akizungumzia kampeni ya 'Namthamini' inayoendeshwa na EATV LTD kuelekea Siku ya Wanawake Duniani Dkt. Tulia amesema kwamba jamii nyingi hazina utaratibu wa kuongea kwa uwazi mabinti kutokana na mila potofu zilizopo katika makabila tofauti nchini.
“Kuna makabila ni mwiko mzazi kuzungumza na binti yake kuhusu masuala ya ukuaji hivyo hata mama kumfundisha binti namna ya kujisitiri kwa njia za kienyeji ni tabu, hapo ndiyo ambapo unamkuta binti anaona bora asiende shule abaki nyumbani mpaka siku za mzunguko wake wa hedhi utakapoisha”. Alisema Dkt Tulia
Pamoja na hayo Dkt. Tulia amekiri umasikini upo juu na hicho ndicho chanzo cha wanafunzi wengi kushindwa kumudu gharama za taulo hizo (Pedi), na kuongeza kuwa kwa maeneo ya vijijini taulo hizo hazipo jambo ambalo linawafanya mabinti wengi kutumia vifaa ambayo kiafya ni hatari.
Dkt. Tulia ameongeza kwamba jukumu la mzazi yoyote yaani baba au mama ni kuhakikisha vijana wanawekwa wazi kinapofika kipindi cha hedhi na balehe, siyo kuendeleza mila potofu ambazo zinaleta madhara kwa baadae ikiwa ni pamoja na kutimiza majukumu ya kifamilia kama kumuandalia binti vifaa vya kujisitiri na siyo kuiachia serikali kwa sababu jambo hilo likiachiwa serikali halitokuwa endelevu.