Imekaaje Hii..Miss Tanzania Ashauri Kuwepo na Somo Maalumu Kuhusu Hedhi Mashuleni...!!!


Miss Tanzania Mwaka 1998, Basila Mwanukuzi  ameishauri serikali kuweka somo la kuwafundisha mabinti namna ya kujihifadhi ngazi ya shule za msingi  kwa kupitia walezi (Matron)  kipindi wanapokuwa wameanza kupata mabadiliko ya ukuaji wa mwili.

Akizungumza leo katika kipindi cha East Africa Breakfast  ya East Africa Radio katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Miss Mwanukuzi amesema kuwa suala linalohusu watoto wa kike kujisitiri linahusu jamii nzima na siyo waachiwe wanawake peke yao.

“Katika suala kujisitiri tusiachiwe wanawake peke yetu, hili ni suala la jamii nzima na hata serikali ina wajibu wa kusaidia mabinti na wadogo zetu kuwapatia masomo ambayo kupitia ‘Matron’ wanafunzi wa shule za msingi watapata mafunzo, kwani siyo kila mmoja anapata mafunzo hayo akiwa nyumbani” - Bi. Mwanukuzi.

Bi. Mwanukuzi amesema mila na desturi potofu ndicho chanzo cha jamii kufanya siri suala la ukuaji na hata kufikia mama kushindwa kuzungumza na binti yake na kwa kuwa kitendo hicho wakati mwingine hutafsiriwa kama ukosefu wa adabu.

Hata hivyo ameweka wazi kuwa wanawake wanapaswa kuinuana ili mambo yanayohusu wanawake waweze kusaidiana wenyewe kwa wenyewe na ndiyo sababu taasisi yake ‘Mwanukuzi Foundation’ imeliangalia suala la kuwainua kina Mama Lishe kwa kuwapatia elimu, kuwafanya watambulike na wathaminiwe zaidi.

Pamoja na hayo Bi Mwanukuzi ameongeza suala la mabinti kusaidiwa vifaa vya kujisitiria wakati wa hedhi lipewe kipaumbele kama suala la madawati na huduma nyingine  na siyo kuachiwa kwa watu wachache.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad