Jennifer Kanumba: Walimu na Wanafunzi Walinitenga Wakidhani ni Mchawi Kweli...!!!!


Staa wa utotoni, Hanifa Daudi maarufu kama Jennifer kwenye filamu za marehemu Steven Kanumba, amedai kuwa siku za mwanzo wakati ameingia kidato cha kwanza, walimu na wanafunzi walikuwa wakimuogopa wakidhani ni mchawi kweli.

Kwenye moja ya filamu za Kanumba, Hanifa aliigiza kama mchawi.

“Vituko vilianza nilipoanza form one nikachukuliwa nikapelekwa boarding iko Same sasa kunipata shida watu walikuwa wananijaalia,” Hanifa alikiambia kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM kinachoendeshwa na Raheem Da Prince.

“Kuanzia walimu hadi wanafunzi walikuwa wananiona mtu wa ajabu labda ntakuwa naringa, mpaka wengine wakawa hawaamini, wanasema naweza nikawa mchawi kweli wakawa wananitenga,” alisema.

“Lakini baadaye sikufanikiwa kuhama nilimaliza pale form four watu walinizoea,” aliongeza.

Hanifa amemaliza kidato cha nne mwaka jana na alipata division two ya 21.

Kwa upande wa mama yake mzazi ambaye anaamini filamu za Kibongo zimekufa tangu kifo cha Kanumba, amesema mwanae yupo wazi kwa atakayetaka kumsimamia kwenye masuala ya filamu ila makubaliano yao yatamhusisha mwanasheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad