Kamanda Wema Sepetu kwenda Arusha kuonana na Godbless Lema



Kamanda Wema Sepetu Jumamosi hii ataelekea mkoani Arusha kwajili ya kuonana na mbunge wa Arusha, Godbless Lema ambaye ameachiwa kwa dhamana Ijumaa hii baada ya kusota gerezaji kwa miezi nne.

Muigizaji huyo ambaye ana wiki moja na nusu ndani ya Chadema toka arudishe kadi ya CCM, amedai kesho atasafiri kwenda mkoani Arusha kuonyesha ushirikiano.

“Mungu ni mkubwa, ni furaha kusikia Mh. Godbless Lema amepewa dhamana. Najua ulipitia wakati mgumu sana, najua ulikuwa mbali na familia yako, watoto wako, rafiki zako, makamanda wenzako na zaidi wananchi wako wa Arusha na Watanzania kwa ujumla. Ni faraja kwetu kwamba sasa umerudi mtaani kuendeleza mapambano,” aliandika Wema Instagram.

Aliongeza, “Kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe, mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke. For that sake, kesho i’ll be in Arusha kuonyesha Solidarity “FOR TO BE FREE IS NOT MERELY TO CAST OFF ONE’s CHAINS, BUT TO LIVE IN A WAY THAT RESPECTS AND ENHANCES THE FREEDOM OF OTHERS” – NELSON MANDELA #CallMeKamanda,”.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aende tu who cares na ampe Nyapu kama anataka vile vile si kwa raha zake

    ReplyDelete
  2. Njoo Kamanda Karibu Arusha na Chaa Arusha kipooo utapata tu,,,,Ila tahadhari usije ukaji babysha kwa Lema ana Mke na watoto wazuri....

    ReplyDelete
  3. Wanafalsafa wanasema, uhuru wako unaishia pale uhuru wa mwenzio unapoanza, hivyo ukivuka mpaka kwa kisingizio cha uhuru wa kutoa mawazo yako, yatakukuta ya Lema. Jitambue sasa, kuwa kwako mahabusu kwa kutukana ni umbumbumbu uliopitiliza ambao unaweza tu kuungwa mkono na mbumbumbu wengine kama Wema. Fight for a cause not nonsense!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad