Keko, Dar: Teja Afariki na Bomba la Sindano ya Madawa ya Kulevya Mkononi...!!!


Hapa DDC Keko, Dar es salaam, kwenye eneo la wazi, katika ukuta unaotenganisha eneo hilo na National Hotel, wakazi wamekusanyika kwa tahayuri baada ya kumuona kijana amelala ukutani na hapumui, inaonekana ameshakufa muda mrefu, kwasababu hata mwili wake umeganda hivyo hivyo alivyo.

Mkononi kijana huyu ana bomba la sindano bado lina ning'inia , kwahiyo inasadikika alikuwa amejidunga madawa ya kulevya.

Majirani waliofika eneo hili, wanasema vita ya Makonda dhidi ya dawa za kulevya inahitajika sana pamoja na mapungufu aliyonayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad