KENYA: Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Peter Munya ametangaza kuwa Serikali itaajiri madaktari kutoka Tanzania, Ethiopia na Cuba ndani ya wiki 3 zijazo.
Madaktari hawa wa kigeni wataajiriwa ili kuchukua nafasi ya madaktari walio katika mgomo uliodumu kwa siku zaidi ya 90 wakidai kuongezewa malipo.
Akiongea katika mkutano huko Naivasha, Munya aliwaambia madaktari ambao bado hawajarudi kazini waende kusaini makubaliano ya utambulisho katika Serikali za Kaunti zao.
Haya yamekuja siku moja tu baada ya Rais Kenyatta kusema kuwa wanachofanya madaktari hao ni 'blackmail' na wanachokitaka ni kikubwa mno na hakiwezi kufanywa ndani ya usiku mmoja.