Katika maadhimisho ya siku ya Sheria nchini alijitokeza Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Swabaha Mohamed Shosi aliyedai kutaka kudhulumiwa na Polisi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mahakama, mbele ya Rais John Magufuli huku akiangua kilio akitaka kusaidiwa. Rais aliomba kusaidiwa kwa mama huyo japo alishindwa keshi. Lakini sasa mambo yamemgeukia.
Kwenye maadhimisho hayo, mama huyo alijitambulisha kwa Rais Magufuli kuwa ni mjane kutoka mkoani Tanga na alidai hali hiyo inatokana na mmoja wa watoto wa marehemu Shosi, Saburia Shosi kuwa ndiye anayepanga mipango ya yeye kudhulumiwa na huku akimtuhumu kuhusika na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Kutokana na tuhuma hizo dhidi yake, Saburia amemburuza mahakamani mama huyo kwa kesi ya kashfa kwa kumhusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Katika kesi hiyo namba 38 ya mwaka 2017, Saburia ambaye anawakilishwa na Wakili Abdon Rwegasira, anaiomba mahakama itamke kuwa tuhuma hizo zilizotolewa na mama huyo dhidi yake ni kashfa.
Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Saburia anadai kuwa yeye ndiye aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa mali za marehemu baba yao, Shosi. Aidha anaiomba mahakama iamuru mdaiwa amuombe radhi na amlipe jumla ya shilingi milioni 400 kama fidia ya madhara aliyoyapata kwa kashfa hizo, riba pamoja na gharama za kesi.
no mtamuonea kwa sababu ni mkenya
ReplyDeleteAnayohaki yakuweka wakili na Kenya wapo MAWAKILI walionaujuzi. .lakini kuchafua jina ameadaiwa millioni 400.ajiandae tu.alisema yuko tayari kufungwa sababu ya kudai haki yake.
Delete