Kimenuka: Serikali Yagundua Bandari Bubu ya Kupitisha Dawa za Kulevya Kisiri


Serikali imewaagiza watendaji wa mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa wanafanya operesheni maalum ya vyombo vya ulinzi na usalama katika eneo la bandari bubu ya Kigombe iliyopo pembeni mwa bahari ya Hindi,baada ya kubaini kuwepo kuwa eneo hilo ndio lango kuu la uingizaji dawa za kulevya,usafirishaji wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya kenya na uvuvi haramu wa mabomu.

Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga,watendaji wa serikali pamoja na wananchi wa eneo la Kigombe,naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi mheshimiwa William Ole Nasha amesema ni lazima operesheni zifanywe kila wakati kwa sababu eneo la Kigombe limebainika kuwa ni kunafanyika uhalifu wa kimataifa ikiwemo kusafirisha binadamu kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Awali mbunge wa jimbo la Muheza mheshimiwa balozi Adad Rajab amesema mbali na uhalifu wa kimataifa kufanyika katika eneo la bandari ya Kigombe,pia vijana wengi wamekuwa wakitumia vyombo vya majini kusafiri na kwenda nje ya nchi na wanapofika huko wanakabiliwa na tatizo la ubebaji na matumizi na utumiaji wa dawa za kulevya.

Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wajumbe wa kamati za ulinzi katika eneo hilo,wameiomba wizara husika kuhakikisha kuwa wanatoa motisha kwa ajili ya kuwawezesha wajumbe kutaja majina ya wavuvi haramu wa mabomu ambao baadhi wanatokea nchi jirani ya Kenya kwa sababu kipato walichonacho na kazi ya kuwataja wahalifu inahatarisha maisha yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad