Kimenukaa..Nape Ahaidi Kujiuzulu Uwaziri Endapo Suala la Makonda Kuvamia Clouds Litamshinda..!!!!


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema endapo atashindwa kusimamia uhuru wa habari na vyombo vya habari nchini atajiuzulu nafasi yake kwa kuwa atakuwa ameshindwa majukumu yake katika nchi huru. 

Nape ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumzia na kulaani kitendo kinachodaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, cha kuvamia chombo cha habari cha Clauds, akiwa na askari wenye silaha na kukifananisha kitendo hicho na kuinajisi taaluma ya habari.

Waziri huyo amesema amezoea kuona matukio kama hayo yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwa bunduki lakini kwa nchi yetu si jambo jema kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki mkononi.

"Tumezoea kuona matukio haya yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki si sawa, kwa jambo hili tunataka kutenda haki tumsikilize Mkuu wa Mkoa ili tujue kwanini amefanya jambo hili". Alisema Nape

Kufuatia tukio hilo Waziri Nape ameunda tume yenye wajumbe takribani watano itakayoenda kumhoji Makonda na kutoa mrejesho wa kazi hiyo ndani ya masaa 24 ikiwa imeeleza sababu maalum kutokea kwa tatizo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad