Kimenukaa..Nape Nnauye Aaanza Kuichana Serikali ..Amtaja Magufuli na Mwakyembe..!!!


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter amempongeza Rais Magufuli kwa kutumia busara kumwachia msanii Nay wa mitego huku akienda mbali na kudai kuwa matumizi ya nguvu kubwa hayana faida yoyote.

“Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!" 

Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia juzi ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.Alikuwa anatuhumiwa kwa kutoa wimbo ambao unaikashifu serikali. 

Hata hivyo, Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, jana mchana alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi  kumuchia huru msanii huyo na kutaka wimbo wake ‘Wapo’ uendelee kuchezwa  kwenye vyombo mbalimbali,

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. amekuchana mwwenyewe maana umeaandika mharo kabisa

    ReplyDelete
  2. Kwanini mmewahi kuandika "matusi hapana" ?
    Au kwa sababu mmejitambua kuwa mlichokiandika ni pumba. Kichwa cha habari hakiendani na maelezo yenu ya £÷&$€==¥$¥=£&+¥#£=£÷£$£ mliyoyaandika. Fitna wakubwa nyie....!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad