Kimenukaa..Polisi Waanza Kamata Kamata kwa Wakazi wa Mabondeni,15 Tayari Wapo Selo..!!!


Watu kumi na tano wamekamatwa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salamu kwa kosa la kukaidi agizo la serikali lililowataka kuondoka maeneo ya mabondeni.

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Saimon Sirro amesema watu hao wamekamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukaidi kuhama maeneo hatarishi na kwamba eneo hilo ni mali ya halmashauri ya manispaa ya Ilala.

Hata hivyo kamanda Sirro amesema hali ya usalama katika jiji la Dar es Salaam imetengamaa, ambapo jeshi hilo limefanikiwa kudhibiti vikundi vya kihalifu.

Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata wezi wa magari na uchunguzi bado unaendelea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad