Kimenukaa,,Thea Afunguka Haya Mazito Kuhusu Yeye Kutegemea Mapedeshee Ili Maisha Yake Yaende..!!!


STAA wa filamu nchini, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka kuwa hana mpango na hategemei mapedeshee  kuendesha maisha yake kwani madhara yake ni makubwa.

Akibonga na Risasi Jumamosi, Thea alisema katika maisha yake hajawahi kutegemea wanaume mapedeshee wamwendeshee maisha yake kwani kuna hasara kubwa kwa sababu mastaa wengi wa kike wanaoishi kwa kuwategemea hujikuta wakiachwa na kurudi chini kabisa hivyo ni funzo kubwa.

“Siwezi na sijawahi kutegemea mapedeshee kuendesha maisha, mastaa wa kike wengi tumewaona wakiendesha magari ya thamani, wakiishi kwenye nyumba nzuri lakini wanapoachwa wananyang’anywa kila kitu, wanafilisika wanarudi chini, mimi tangu nimetengana na Mike Sangu sijawahi kumwanika mwanaume yeyote kwamba ni mpenzi wangu,” alisema Thea.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad