Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa siku 14 kwa Shirika la Visiwani Zanzibar (ZECO) kulipa deni lote la ankara za umeme wanalodaiwa na endapo halitafanya hivyo basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kukatiwa umeme.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt. Tito Mwinuka alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hadi kufikia mwezi Januari mwaka 2017, Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) lilikuwa linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 127.8.
“Shirika la umeme linashindwa kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa wakati ikiwemo uendeshaji wa shirika, matengenezo ya miundombinu pamoja na utekelezaji wa miradi, hayo yote yanasababishwa na malimbikizo ya madeni kwa wadaiwa sugu hivyo tunatoa siku 14, wasipoweza kulipa tutawakatia huduma ya umeme”. Alisema Dkt Mwinuka
Aidha mbali na ZECO, Tanesco imewataja wadaiwa sugu wengine ikihusisha Wizara na Taasisi za serikali zikiwa zinadaiwa zaidi ya bilioni 52.5, makampuni binafsi pamoja na wateja wadogo wanaodaiwa zaidi ya bilioni 94.9
Kwa upande mwingine Dkt. Mwinuka amesema shirika hilo linatarajia kuanza oparesheni maalum ya kukusanya madeni hayo na matarajio yao ni kulipwa kwa malikimbizo yote ili yalisaidie kujiendesha kiushandani na kwa ufanisi mkubwa zaidi na kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegema nishati ya umeme nchini.
Hatua hii imekuja ikiwa ni takriban siku 4 tangu Rais Magufuli kuagiza TANESCO kufuatilia madeni yote ikiwemo deni ambalo TANESCO inalidai ZECO, na kuitaka kuwakatia umeme wote watakaoshindwa kulipa kwa wakati.
Tanzania tusichezee moto tuliousababisha wenyewe.zanxibar ya muungano wa vipi.kuna wakati wakutoa makali lakini msjadiliano ni usawa na si amri.ukimlazimisha mtoto kila siku atakugeukia mwenyewe. Mlilazimisha CCzm Zanzibsr. Mkawaacha bila uongozi, amri ilitoka bara mkamweka raisi wenu. Leo mnamzimia umeme kwa ubabe.uongozi wa kibabe una madhara yake.
ReplyDeleteMuungsno wa kulazimisha kwa nguvu ni kaa la moto.na sasa yule raisi wa kulazimidhwa kashindwa kuwahudumia Wazanzibari. Je uhuru, muungano na amani vinalazimishwa.?
Busara wapi. Haya ni mambo tete sasa kwa Taifa. Hili jambo linahitaji hekima na busara kubwa toka kwa viongozi.Mama Samia unaunga mkono Wazanzibari wstendewe hivi.