Kuhusu Nape Nnauye, CUF kutangaza hatua nzito


TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI


Chama cha Wananchi CUF kimepokea taarifa ya hatua ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kumuondoa Mheshimiwa Nape Nnauye katika nafasi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwa mshtuko na masikitiko makubwa.


Mhe. Nape ameondolewa kwenye Baraza la Mawaziri kibabe na bila aibu kutokana na kusimamia Haki, Uhuru, Uwajibikaji, Nidhamu na Maadlili ya uendeshaji wa vyombo vya habari nchini jambo ambalo ni jukumu la msingi la Wizara yake.


Sote tunatambua kwamba Utenguzi huo unatokana na Mhe. Nape kufuatilia tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha Clouds Media Group kinyume na taratibu, maadili na Nidhamu ya utendaji wa majukumu yake. kitendo hicho pia ni kosa la jinai lisilovumilika.


Kwa niaba ya Chama cha Wananchi CUF, napenda kutumia fursa hii kulaani mwenendo wa Rais Magufuli wa kuitumia nafasi yake kwa namna inayokosa BUSARA na HEKIMA ya uongozi kwa TAASISI ya URAIS.


Kitendo cha Rais kumlinda mtuhumiwa ambaye amefanya makosa ya wazi kabisa kinadhihirisha namna Rais asivyo na utayari wa dhati na uwezo wa kusimamia nidhamu ya watendaji serikalini.


Huko nyuma na mara kadhaa, Rais Magufuli alichukua hatua za haraka sana kuwafuta kazi watumishi na watendaji wa serikali waliofanya makosa madogo mno hata kama ilikuwa ni kimatamshi tu au maamuzi ya bahati mbaya.


Mifano mizuri ni pamoja na Mhe. Anne Killango (aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga), Dr. Mwele Malecela (aliyekuwa anaongoza taasisi muhimu ya utafiti wa magonjwa ya binadamu), Wilson Kabwe (Mkurugenzi wa Jiji la Dar Es Salaam) ambaye alituhumiwa mkutanoni na kufukuzwa hapo hapo bila kuwepo wala nafasi ya kujitetea.


The Civic United Front (CUF) inashangazwa na maamuzi ya sasa ya Rais Magufuli ya kumlinda mtuhumiwa wa makosa makubwa na ya wazi kabisa na kisha kumfukuza kazi Waziri aliyekuwa akitekeleza wajibu wake ili kulinda heshima ya serikali.


Kwa kitendo hiki cha Rais, CUF inaungana na watanzania wote kuamini kuwa Rais Magufuli hana nia njema ya kurejesha nidhamu serikalini, na kwamba yuko tayari kuwalinda vijana wake wachache kuliko kuilinda serikali na heshima ya nchi na Taasisi ya Urais. Rais anashusha hadhi ya Ikulu na sasa ikulu imegeuka kuwa mtetezi mkuu wa watumishi waovu wa umma.


CUF itatangaza hatua nzito hapo baadaye, kwa niaba ya chama natumia fursa hii kumfariji na kumtia nguvu Mhe. Nape kwa ujasiri aliouonyesha na kusimamia kile ambacho ni haki kwa Taifa, wananchi na sekta ya habari.


Namuomba asirudi nyuma kutetea haki za watanzania wote na kamwe asikatishwe tamaa na kitendo hicho kilichokosa utu na heshima, na kujali mchango mkubwa wa kisiasa ndani ya Chama chake na serikali ya awamu ya Tano.


CUF inaungana na watanzania wote kulaani kitendo hicho na kwamba tutakutana pia na vyama washirika katika UKAWA ili kuamua hatua kubwa za pamoja dhidi ya ukosefu wa haki na Demokrasia nchini na matumizi mabaya ya mamlaka.


"CUF NI TAASISI IMARA YENYE VIONGOZI MAKINI"

HAKI SAWA KWA WOTE


JULIUS MTATIRO

MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI 

CUF-TAIFA.

23 Machi, 2017.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyinyi CUF mnajiingiza ktk matatizo au mabadiliko ya CCM yakwenu yamewashinda kama kutoana roho waachieni wanaccm msiwachagulie huyu mzuri huyu mbaya kwanza jitazameni yakwenu siasa za maji taka za matukio ya ccm tumezichoka

    ReplyDelete
  2. Wala unga ndie wanapiga kelele na kejeli kwa kazi ya iliyokuwa na umakini aifanyayo Raisi alisema sasa sio wakati wa udaku ni kufanya kazi na huyo Mtatiro na NAPE mgewashauri clouds kama wamevamia wangeripoti polisi sio kulishikia bango kwenye media wakati kuna kazi ngumu ya kukabiliana na mapapa ya unga

    ReplyDelete
  3. toa kibanzi kilicho nani ya jicho lako ndipo .......................................... mtatiro

    ReplyDelete
  4. Yakwenu yanawashinda , mnavalia njuga haraka-haraka yasiyowahusu....hovyooooo,

    ReplyDelete
  5. Rais wangu Ni magufuri sina Raisi mwingine WA nchi

    ReplyDelete
  6. kwa Hiyo kuna CUF- TAIFA - CUF-ASILIA- CUF - BARA - CUF MATATIZO- CUF-VISIWANI - CUF-WAZALENDO- CUF-SULTANI- CUF-WALALA HOI.

    CUF- RUZUKU
    CUF - PLOFESA
    CUF - MAALIM
    CUF- MTATIZO
    CUF- ILE ILE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad