Kwa Mara ya Kwanza Leo..Wema Sepetu Atapanda Jukwaa la Chadema Kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mhe Godbless Lema Arusha...!!!!


Malkia wa filamu Wema Sepetu atahudhuria mkutano wa hadhara Ijumaa hii wa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mhe. Godbless Lema utaofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ngarenaro Arusha jioni ya leo.

Mbunge huyo itakuwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza na wananchi wake ikiwa ni siku chache toka aachiwe na mahakama kwa dhamana baada ya kukaa rumande miezi 4.

Muigizaji huyo tayari yupo Arusha, jana ametoa taarifa kwamba ameshafika katika mji huo kwajili ya mkutano huo ambao unatarajiwa kuwa na watu wengi.

“Glory Be to God…!!! I had a safe Travel…! Back in Arusha ready for tomorrow’s Meeting with Hon. Godbless Lema… Y’all better be there… Im sure he’s got alot to share with Us… Goodmorning World…. Kajua kanapiga,” aliandika Wema Instagram.

Wema pamoja na mama yake walihamia CHADEMA mwezi mmoja uliopita baada ya kudai kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya viongozi wa chama cha CCM.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad