Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesomewa mashtaka matano na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi likiwamo ya kutoa maneno yenye nia ya kuhimiza hisia za kidini ambayo yangeweza kupelekea uhasama baina ya jamii za Watanzania.
Lissu amekana mashtaka yote na upande wa mashtaka umedai upelelezi umekamilika na wameomba wamsomee maelezo ya awali leo (Ijumaa).
Lissu ambaye anajiwakilisha yeye mwenyewe mahakamani hapo aliomba maelezo hayo ya awali yasomwe Jumatatu, ili aweze kuhudhuria uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) unaotarajia kufanyika kesho.
Ameomba apewe dhamana kwa masharti nafuu.