Lowassa Ampa 'Makavu Live' Rais Magufuli,Amataka Afute Kauli Lasivyo...!!!!


WAZIRI Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amemwomba Rais Dk. John Magufuli kufuta kauli yake ya kuwazuia wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  kushirikiana na wabunge wa upinzani.

Akizungumza jana katika ziara viongozi wa Chadema katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, Lowassa alisema kauli hiyo Rais Dk. Magufuli inabomoa misingi ya amani iliyojengwa na waasisi wa taifa letu.

'”Namuomba Rais (Magufuli)  aondoe kauli ile aisahihishekauli hiyo na nawaomba watanzaniatukatae kugawanywa…tusikubali nchi hii ni yetu sote hakuna mtu mwenye haki miliki hapa ikienda vibaya tunaangamia wote ikienda vizuri tunafaidi wote kwahiyo tukatae,” alisema

Alisema Watanzania wamekuwa wakiishi bila ya kubaguana kwa misingi ya dini, rangi au ukabila na kukumbushia kauli iliyowahi kutolewa na baba wa taifa kuwa ubaguzi ni sawa sawa na kula nyama ya mtu, ukishakula hutotaka kuiacha.

Mjumbe wa huyo wa Kamati Kuu alisema hali ya maisha imezidi kuwa ngumu, huku bei ya bidhaa ikizidi kupanda kila siku.

Kutokana na hali hiyo alisema CCM kiliiba sera ya Chadema, ikiwemo elimu bure, lakini imeshindwa kuitekeleza.

“'waliiba sera na ilani yetu ya uchaguzi, lakini kwa kuwa hawakujiandaa wamefanya hali kuwa ngumu sana,” alisema

Katika kikao hicho cha ndani cha kuimarisha chama, Lowassa ameeleza tatizo la ajira linavyozidi kuwa kubwa na kuongeza kuwa mipango mibovu imesababisha sekta binafsi kuyumba, huku makampuni kadhaa na shughuili nyingine za kutoa ajira zikifungwa na kusababisha ongezeko kubwa la wasiyo na ajira.

Kuhusu ushirikiano miongoni mwa vyama vya upinzani, Lowassa alisema Ukawa ni muhimu kuliko wanavyoweza kudhani kwani muunganiko wa vyama vya siasa katika karne hii ni jambo la muhimu.

“Kikubwa cha kuzingatia ni umoja na mshikamano. Watanzania wana imani kubwa sana na chadema kwa sasa na kama kuna mtu anatafuta chama mbadala cha kuhamia basi ni Chadema,” alisema 

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CHAMA CHA KUHAMIA SASA HIVI NI ACT WAZALENDO,CHADEMA MPOMPO TU.

    ReplyDelete
  2. Sasa tunaenda kubaya kama ndiyo kutukata chungwa kimtindo huo!! VIP? Watu wameowana, ndugu. Majirani. Heeee likibuma yy yuko state houseeee.

    WaTanzania tuache nizamu ya woga tupinge utengano huu

    ReplyDelete
  3. Lowasa afute kwanza yeye kauli yake aloitoa kwamba Waluteri hawajatoa Raisi kama Wakatoliki, na huo nao ni ubaguzi wa kidini, ni mbaya kuliko............
    Hata hivyo JPM alimzungumzia Lema peke yake, kwani adui wa baba yako ni adui yako pia, haiwezekani adui wa baba yako awe rafiki yako, huyo baba atakuamini kweli??

    ReplyDelete
  4. Magufuli rais wa kweli, Lowasa anahitaji wafuasi waongezeke cdm kama nikihitaji kuhama naenda kwa WAZALENDO ACT! Alionesha nia ya kuwa mwenyekiti CDM akafukuzwa na wewe jaribu kuutaka uenyekiti ukione kilicho mfanya mtema kuni ateme kuni. ACT-CCM.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad