Ukiisikia simulizi ya Makonda, alipotoka, alipo na anapokwenda, mtakubaliana na mimi kuwa hii ni kazi ya Mungu katika kuonyesha uwezo wake kwa wanadamu kwa kuufanya muujiza wa Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni.
Historia Yake Kuzaliwa na Familia
Makonda alizaliwa Februari 15, 1982 majira ya saa 1:30 asubuhi, familia ya mzee Makonda (Baba hatajwi majina) na mkewe, Suzan, walimkaribisha mtoto wao pekee wa kiume katika Zahanati ya Kolomije, wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Elimu ya Msingi, Sekondari na Chuo.
Makonda ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi. Kabla ya kwenda Moshi, alipita katika Shule ya Msingi Kolomije na amesoma pia katika Chuo cha Uvuvi, Mbegani, Bagamoyo ambako alisoma hadi ngazi ya Diploma katika masuala ya uvuvi.Hakuna maelezo alisoma wapi Sekondari wala hakuna index number yoyote ya Necta yenye majina yake.
Kabla ya Chuo.
Makonda alianzia kazi ya kuchimba mchanga.
Akaja kazi ya kuchoma mkaa.
Akawa utingo kwenye mabasi stendi
Kisha akawa kondakta yaani Makonda akawa konda.
Ukiwa ni mpakwa mafuta kama Daudi, Mungu atakuinua kutoka chini ulipo na kukupandisha mahali pa juu palipo inuka.
Mibaraka.
Mibaraka kwa Makonda ilianzia siku yake ya kuzaliwa February 15, mwaka 2015 Rais Jakaya Kikwete alipomteua Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na kutangazwa Februari 18, mwaka 2015. Kuteuliwa siku yako ya kuzaliwa sio coincidence bali ni mipango ya Mungu.
Mibaraka Zaidi.
Hii ni kazi ya mikono yake kwa baraka za Bwana. (Not necessarily ni kweli)
Inasemekana Mungu amemuwezesha
Makonda kununua jengo (apartment), pale Viva Towers kwa Sh600 milioni. Makonda amempa mke wake gari aina ya Mercedes Benz lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani (Sh550 milioni) kama zawadi ya ‘Birthday’,”
Makonda ana gari aina ya Lexus, lenye thamani ya Sh400 milioni. Makonda anamiliki magari mengine ya kifahari aina ya V8, anajenga maghorofa jijini Mwanza na amekarabati ofisi yake kwa Sh400 milioni zake binafsi.
Japo there is something missing ambayo ni a missing link kwenye story ya Makonda ambayo wazazi hawajaisema, Makonda mwenyewe hajaisema, wala sijaisikia ikisemwa popote, kuhusu elimu ya Sekondari, the bottom line ni the end justify the means.
Huwezi jua!.
Mwacheni Mungu aitwe Mungu.
Paskali
Alie mueka ndie atakae mtoa kila mtu na. bahati yake msomkalie rohoni mwenzenu chaaaaa
ReplyDelete